Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ali Kamwe aanguka na kuzirai akishangilia ushindi dhidi ya CR Belouizdad

Kamwe Hospital 0004 Ali Kamwe azirai akishangilia

Sat, 24 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati mashabiki wa Yanga wakishangilia ushindi wao baada ya kuichapa CR Belouizdad kwa mabao 4-0 hali sio nzuri kwa Ofisa habari wake, Ali Kamwe ambaye ameanguka na kupoteza fahamu baada ya mchezo huo kumalizika.

Kamwe amekumbana na hali hiyo leo Februari 24, 2024 katika Dimba la Benjamin Mkapa wakati akishangilia ushindi huo kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ambapo ameanguka na kupoteza fahamu.

Kamwe amechukuliwa na kutolewa nje vyumba hivyo kisha kupelekwa hospitali huku akiendelea kupatiwa matibabu akiwa ndani ya gari la wagonjwa.

Katibu wa Madaktari wa Tiba za Wanamichezo nchini, Dr Juma Sufian amethibitisha tukio hilo huku akiomba apewe muda kwani yupo kwenye harakati za kumsaidia msemaji huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live