Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ali Kamwe: Ukweli ni kwamba Aziz Ki hatunaye

Aziz Ki WA0000 Aziz Ki

Wed, 22 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga imethibitisha kuwa nyota wake, Stephanie Aziz Ki mpaka sasa bado hajasaini mkataba wowote ndani ya klabu hiyo licha ya mkataba wake wa awali kuelekea ukingoni mwishoni mwa msimu huu.

Akithibitisha hilo, Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe amesema kuwa yeye hafanyi propaganda wala kuwahadaa mashabiki wao lakini uhalisia ni kwamba mchezaji huyo hajasaini mpaka sasa.

"Wanaomuhitaji Aziz Ki wapo vizuri kifedha hiyo ni kweli sina haja ya kuleta propaganda mimi nimenyooka kama rula, mimi ningekuwa mtu wa propaganda ningewaambia Aziz kasaini ila ukweli bado hatunae, hakuna siasa hapa tusipeane moyo wakati uhalisia tunaukimbia.

"Kama hatutakuwa na pesa hatutaweza kumzuia Aziz KI abakie Yanga, Wanachama wa Yanga mnatakiwa mlipe Ada na mjisajili na sio kuuliza Aziz Ki anaondoka Yanga au anasalia Yanga," amesema Ally Kamwe.

Vilabu vya Mamelodi Sundowns, Al Ahly, ES Tunis, Pyramids FC, Orlando Pyrates, Kaizer Chiefs na vingine vingi vinatajwa kuweka mpunga mrefu ili kuinasa saini ya nyota huyo raia wa Burkina Faso ambaye kwa sasa anaongoza kwa upachikaji mabao ndani ya Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live