Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Algeria mabingwa FIFA Arab Cup 2021

Algeria 1 1024x682 1 Mabingwa wa FIFA Arab Cup 2021

Mon, 20 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Taifa ya Algeria imefanikiwa kutwaa ubingwa wa FIFA Arab Cup 2021 baada ya kuifunga Tunisia 2-0 katika fainali iliyoenda katika muda wa nyongeza (dakika 120).

Magoli ya Amr Sayoud (dk 99′) na Yacine Brahimi (dk 120+5) walioingia wakitokea benchi yaliwahakikishia Algeria ubingwa katika dimba la Al Bayt hapo jana.

Sayoud, 31 alicheza mechi ya kwanza ya ufunguzi wa mashindano hayo na hakucheza tena mpaka hapo jana alipocheza katika dakika 60 za mwisho za mtanange huo.

Mashindano hayo ya FIFA Arab Cup yamechukuliwa kama maandalizi ya finali za Kombe la Dunia 2022 litakalo chezeka Qatar mwezi November.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live