Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Algeria kuwa mwenyeji wa mechi za timu ya taifa ya Palestina

Algeria Kuwa Mwenyeji Wa Mechi Za Timu Ya Taifa Ya Palestina Algeria kuwa mwenyeji wa mechi za timu ya taifa ya Palestina

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Algeria inasema kuwa itakuwa mwenyeji wa mechi zijazo za timu ya taifa ya Palestina kufuatia ombi la Chama cha Soka cha Palestina.

Palestina imeratibiwa kuanza kampeni ya Kombe la Dunia la 2026 katika kanda ya Asia mwezi ujao.

Mechi yao ya kwanza ya kufuzu, ugenini dhidi ya Lebanon tarehe 16 Novemba, itachezwa katika Falme za Milki ya Kiarabu.

Mechi ya 'nyumbani' dhidi ya Australia siku tano baadaye inaonekana itachezwa kaskazini mwa Afrika.

Kufuatia shambulio dhidi ya Israel na kundi la wanamgambo wa Hamas tarehe 7 Oktoba, ambalo lilisababisha vifo vya zaidi ya watu 1,400, eneo la Gaza limekuwa likikabiliwa na mashambulizi ya anga ya kulipiza kisasi, ambayo yamesababisha vifo vya takriban watu 3,000, huku Waisraeli wakitarajia kuanzisha mashambulizi makali ya ardhini.

"Rais wa Shirikisho la Soka la Algeria, Bw Walid Sadi, anatangaza kwamba nchi yetu itakuwa mwenyeji wa mechi rasmi ya Palestina-Australia, iliyopangwa kufanyika Novemba," shirikisho la Algeria liliandika kwenye tovuti yake.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa uamuzi wa kuandaa "mechi zote rasmi na zisizo rasmi kama sehemu ya maandalizi ya timu ya soka ya Palestina kwa Kombe la Dunia la 2026 na kufuzu kwa Kombe la Asia 2027" ulichukuliwa "kulingana na mamlaka inayoongoza ya Algeria".

Shirikisho la Algeria limeongeza kuwa litalipa gharama zote, kama vile usafiri na malazi, zinazohusiana na timu ya Palestina.

Chama cha Soka cha Palestina, ambacho uwanja wake wa kitaifa uko Ukingo wa Magharibi, kimetafuta usaidizi kutoka nje huku mzozo wa eneo hilo ukizidi, kikisema kwamba Shirikisho la Soka la Asia limelitaka kuandaa mechi ya Australia katika uwanja usio na upande wowote.

Chanzo: Bbc