Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alexander Isak, Arsenal mambo bado ni magumu

Alexander Isak. Asdc Straika wa Newcastle United na timu ya taifa ya Sweden, Alexander Isak

Thu, 6 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Straika wa Newcastle United na timu ya taifa ya Sweden, Alexander Isak ambaye anahusishwa sana na Arsenal amesisitiza hana mpango wa kuondoka kwenye timwu hiyo kwa sasa na anajisikia furaha kuendelea kuwa hapo.

Isak mwenye umri wa miaka 24, ni mmoja kati ya washambuliaji walioonyesha kiwango bora kwenye Ligi Kuu England msimu uliomalizika na alicheza mechi 40 za michuano yote na kufunga mabao 25.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amependekeza jina la staa huyu mwenye asili ya Eritrea kutokana na mapungufu yaliyopo kwenye eneo lao la ushambuliaji msimu uliomalizika.

Mkataba wa sasa wa fundi huyu unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.

Newcastle iliripotiwa kuwa tayari kumuuza Isak ili kubalansi vitabu vyao vya mahesabu na kuepuka rungu kutoka mamlaka za soka nchini England kwa kukiuka sheria za matumizi ya pesa.

Newcastle ambayo msimu ujao itashiriki michuano ya Ulaya ya Ueropa Conference haina presha na inachotaka ni kuuza na kununua mastaa wengine watakaoifanya timu itishe zaidi na uwezekano wa Isak kuondoka pesa ikiwekwa mezani ni mkubwa.

KOCHA mpya Liverpool Arne Slot amependekeza jina la beki wa Feynoord Lutsharel Geertruida, 23, na kutaka asajiliwe dirisha hili. Staa huyu wa kimataifa wa Uholanzi huduma yake pia inahitajika na Tottenham, Newcastle na West Ham. Slot amependekeza jina la staa huyu kwa sababu anamfahamu vizuri kwani amewahi kumfundisha akiwa Feynoord msimu uliomalizika na alionyesha kiwango kizuri.

DALILI zote zinaonyesha huenda Manchester United ikafanikisha mchakato wao wa kumsajili beki kisiki wa Everton Jarrad Branthwaite katika dirisha hili baada ya timu yake kuanza kutafuta mbadala wake ambapo kwa sasa wapo kwenye mazungumzo na beki wa Sheffield United Max Lowe ambaye anatarajiwa kuwa huru katika siku chache zijazo. Safu ya kiungo ya United msimu uliopita iliruhusu mabao ndio maana inasaka mabeki.

KOCHA wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amezungumza na beki wa timu hiyo Nacho, 34, na kumtaka afikirie upya uamuzi wake wa kutaka kuondoka kwani bado anamhitaji kwenye timu. Nacho alikutana na mabosi wa Madrid wiki hii kwa ajili ya kufanya majadiliano juu ya hatma yake kwenye timu hiyo wakati mkataba wake wa sasa ukitarajiwa kumalizika mwisho wa mwezi huu.

BARCELONA inaangalia iwezekano wa kumsajili kiungo wa Real Sociedad, Mikel Merino katika dirisha hili baada ya kuvutiwa na kiwango alichoonyesha tangu kuanza kwa msimu uliomalizika. Merino mwenye umri wa miaka 27, msimu uliopita amecheza mechi 45 za michuano yote amefunga mabao nane na kutoa asisti tano. Mkataba wake unamalizika mwaka 2025 na huenda akaondoka.

MANCHESTER United imeendelea kufanya mazungumzo na Jonny Evans kwa ajili ya kumsainisha mkataba mpya utakaomwezesha kubakia kwenye kikosi cha mashetani hao wekundu kwa muda mrefu. Mbali ya Evans, Man United pia ipo katika mazungumzo na kipa wao namba mbili Tom Heaton. Mbali ya kutaka kuwabakisha wakongwe hao Man United pia inahitaji kumwachia Brandon Williams.

TOTTENHAM na West Ham zinapambana kwa ajili ya kuipata saini ya straika wa Sevilla, Youssef En-Nesyri katika dirisha hili. Staa huyu wa kimataifa wa Morocco mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu huu na haonekani kuwa na mpango wa kusaini tena hali inayosababisha Sevilla kutaka kumuuza ili asiondoke bure.

BENFICA imekataa ofa ya Pauni 51 milioni kutoka Manchester United inayohitaji saini ya kiungo wa Joao Neves katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Mabosi wa Benfica wapo tayari kumuuza fundi huyu wa kimataifa wa Ureno lakini kwa kiasi cha pesa kitakachokuwa kikubwa.

Neves ni mmoja kati ya mastaa tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Benfica.

Chanzo: Mwanaspoti