Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alex Ngereza: Yanga hawakuwa bora kuliko Simba

Alex Ngereza Vs Yanga Nov 5 Alex Ngereza: Yanga hawakuwa bora kuliko Simba

Mon, 6 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati wadau na wachambuzi mbalimbali wa Soka wakisifu ubora wa Yanga waliouonesha katika mchezo wa Dabi ya Karikoo jana Novemba 5 na kuibuka na ushindi wa mabao 5-1.

Mchambuzi wa Michezo kutoka TV3 Alex Ngereza amesema kuwa sio kweli kwamba Yanga walikuwa Bora kuliko Simba katika mchezo huo.

Ngereza anasema;

"Guys sio kwamba Yanga walikuwa bora sana kuliko Simba ila Simba wamefanya makosa mengi kwenye maeneo hatari na kama Simba wangecheza kama ambavyo walicheza dhidi ya Al ahly hapa Nyumbani na kule ugenini Simba wasingefungwa magoli mengi kiasi hiki

Angali magoli mfano goli la nne Max Nzegeli amekutwa na mpira akiwa peke yake kabisa na ukiacha goli hilo angalia tena goli penalty Inonga ameenda kufanya tackling vibaya akamgusa mtu badala ya kugusa mpira

Makosa kama haya ambayo Simba wamefanya leo dhidi ya Yanga ilikuwa lazima waadhibiwe Kutokana na ubora wa wachezaji waliopo kwenye kikosi cha yanga"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: