Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alex Ngereza: Wanaogopa kumpa "Thank you" ataibukia Simba

Ngereza X Bangala Alex Ngereza akimzungumzia Yannick Bangala

Tue, 25 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati sakata la wachezaji wawili wa Yanga Djuma Shaban na Yannick Bangala likiwa bado halijajulikana mwisho wake.

Watu wameendelea kuhoji kwa nini nhasa Klabu ya Yanga imekuwa kimya kuhusiana na taarifa za wachezaji hao.

Fununu zinasema kwa Djuma Shaban yeye anataka kutolewa kwa Mkopo TP Mazembe lakini amegoma akitaka kuvunjiwa Mkataba na Bangala anataka kutolewa Singida FG nae pia akigoma akitaka kuvunjiwa Mkataba.

Sasa Mchambuzi wa michezo kutoka TV3 Tanzania Alex Ngereza ameeleza sababu kwa nini mchezaji kama Yannick Bangala Yanga wamekuwa na kigugumizi katika maamuzi ya kuvunja Mkataba wake ambao unaisha mwakani 2024.

Ngereza anasema kwa uwezo wa Bangala akipewa 'Thank you' Yanga ni jambo rahisi kuibukia kwa watani zao Simba SC na ndio kitu ambacho Yanga hawakitaki.

"Kwa ubora alionao Bangala yaani Yanga wakimpa Thank You tu leo kesho anasajiliwa Simba au Azam hakuna sehemu ambayo atakosa namba na hiko ndio wanachokihofia Yanga kutangaza kuachana nae hasa kipindi hiki cha usajili kwa sababu wanajua madhara yake"

Je ni kweli Bangala anaweza kupata namba katika vikosi vya Simba na Azam FC? Tupe maoni yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: