Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alex Ngereza: Musonda hawezi kuwafikisha Yanga popote pale

Ngereza X Musonda Alex Ngereza amchambua Kennedy Musonda

Mon, 24 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Yanga ikiwa katika wakati mgumu wa kuachana na Mshambulaiji wake kinara Fiston Mayele.

Wapo baadhi ya wachambuzi wa Soka nchini waliotaka timu hiyo kutokuwa na wasiwasi na badala yake wampe nafsi Kennedy Musonda atawapa sawasawa na kile alichokuwa anawapa Fiston Mayele.

Sasa hilo ni tofautik wa mchambuzi Alex Ngereza kutoka TV3 Tanzania ambae yeye anasema Musonda sio Mshambuliaji wa kariba ya Mayele na watakuwa wamefanya kosa kubwa sana wasipofanya usajili wa Mshambuliaji wa kati.

Akizungumza ngereza anasema;

"Kennedy Musonda sio mshambuliaji mwenye uwezo wa kuibeba Yanga msimu ujao, watafute mshambuliaji mwingine haraka kabla dirisha la usajili halijafungwa"

"Wapo washambuliaji wazuri ambao wanatamani sana kucheza Tanzania yupo Cesar Manzoki wanaweza kumpata kirahisi kwasababu mwenyewe hafurahii kucheza huko uarabuni kama wataendelea kumtagemea Musonda sioni kama wanaweza kufanya vizuri."

Je Mwananchi unazungumziaje mtazamo wa Alex Ngereza? Tupe maoni yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: