Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alex Ngereza: Aziz KI ni mchezaji mvivu sana, atakosa namba kwa Gamondi

Alex Ngereza X Aziz Ki Mchambuzi wa Michezo Alex Ngereza akimzungumzia Aziz KI wa Yanga

Mon, 7 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Yanga ikiondokewa na mchezaji wake muhimu kikosini aliekuwa anaanza katika kikosi cha wachezaji 11.

Mashabiki wengi wameonekana kugawa majukumu kwa nyota wenye majina makubwa na uwezo mkubwa waliobaki kikosini humo.

Miongozi mwa nyota wanaotajwa kuwa na uwezo mkubwa ni Aziz KI ambae wapenda kandanda wanaona kuwa iwapo atatimiza majukumu yake uwanjani ipasavyo na kushirikiana na nyota wapya waliosajiliwa kikosini basi ni ngumu kuona pengo la mayele alietimkia FC Pyramids ya Misri.

Sasa mchambuzi wa Michezo kutoka TV3 Alex Ngereza amekuwa na la kusema juu ya mitazamo ya wanaomsema Aziz KI;

"Aziz Ki sio mchezaji mbaya lakini changamoto yake kubwa mvivu anapokuwa uwanjani anashindwa kwenda sambamba na mikimbio ya wachezaji wenzake na iwapo ataendelea na tabia hii anaweza akakosa namba kwenye kikosi cha kwanza msimu ujao"

Mwananchi unauzungumziaje mtazamo wa Alex Ngereza? Toa maoni yako

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: