Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alcantara kuondoka Liverpool

Thiago Alcantara Liverpool Alcantara kuondoka Liverpool

Thu, 28 Dec 2023 Chanzo: Dar24

Uongozi wa Liverpool unadaiwa kuwa tayari kumuuza kiungo wao, Thiago Alcantara dirisha lijalo na baadhi ya timu kutoka Saudia zimeonyesha nia ya kumsajili.

Thiago ambaye tangu kuanza kwa msimu huu hajacheza mechi yoyote, dirisha lililopita Al Ahli ilijaribu kumsajili kwa kuweka ofa ya Euro 12 milioni.

Mkataba wa staa huyu unamalizika mwisho wa msimu na Liverpool haionekani kuwa na mpango wa kumsainisha tena hivyo wanafikiria kuchukua pesa badala ya kumshuhudia akiondoka bure mwisho wa msimu.

Pia Ripoti kutoka tovuti Football Espana, zimeeleza Alcantara anaweza akabadilisha maamuzi na kuamua kurudi nchini Hispania ikiwa atapata ofa nzuri kutoka kwenye timu mojawapo ingawa inaonekana kuwa ngumu kutokana na rekodi yake ya majeraha ya mara kwa mara.

Vilevile huenda akatimkia Saudia kwa sababu ya pesa ndefu anazoweza kupata kutoka kwa matajiri hao.

Chanzo: Dar24