Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alala na Jezi ya Messi kwa miezi mitatu bila kuifua

Vergas Messi Jezi Alala na Jezi ya Messi kwa miezi mitatu bila kuifua

Thu, 14 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Winga wa zamani wa klabu ya Espanyol Matias Vargas,26, amefichua kuwa alilala na jezi ya Lionel Messi bila kuifua kwa miezi mitatu baada ya kuipata jezi hiyo walivyobadilishana uwanjani.

Mwaka 2020 Vargas akiwa Espanyol, walikuwa wanacheza na Barcelona, Vargas akaingia kipindi cha pili kwenye mchezo huo ulioisha kwa sare ya 2-2. Baada ya mechi Vargas akafanikiwa kubadilishana jezi na Murgentina mwenzake Lionel Messi.

Akiongea na Fox Sports, Vargas amesema : “ Nililala na jezi Messi karibu na mto wangu kwa miezi miwili au mitatu. Vile vile chafu ilivyokuwa. Nilicheza dhidi yake na tukabidilishana jezi. Mama yangu akaniamba ‘Acha niifue’. Nikamwambia asiiguse.”

Vargas kwa sasa anachezea Klabu ya Shanghai Port ya ligi kuu nchini China.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live