Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Al Merreikh atapigwa huko huko Rwanda

Yanga Merreikh A0013 Al Merreikh atapigwa huko huko Rwanda

Tue, 5 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga haina hofu kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza ligi ya mabingwa Afrika kuwania tiketi ya kutinga makundi dhidi ya El Merrikh ya Sudan

Kwanza mchezo huo kupigwa Rwanda ni habari njema kwa Yanga kwani inaaminika kuwa Yanga itapata uungwaji mkono nchini humo kutokana na historia yake

Raisi wa Rwanda Paul Kagame ni mdau mkubwa wa michezo na inaaminika kuwa ni shabiki mkubwa wa Yanga.

Mwaka 2012 Raisi Kagame aliialika Yanga nchini Rwanda baada ya kuwa imetwaa taji la Kagame. Hii mialiko ya maraisi kwa Wananchi imeanza siku nyingi.

Pamoja na kuwa Yanga itapata mashabiki wengi nchini Rwanda lakini pia Wananchi wana kila sababu ya kutembea kifua mbele kutokana na ubora wa kikosi chao kuelekea katika mchezo huo. Yanga wamesheheni wachezaji wengi vijana wenye uwezo mkubwa na uzoefu wa kutosha.

Djigui Diarra, Yao Kouassi, Joyce Lomalisa, Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Khalid Aucho, Jesus Moloko, Mudathir Yahya, Kennedy Musonda, Stephanie Aziz Ki, Maxi Nzengeli, Skudu Makudubela, Pakome Zouzoua na wengine wengi ni wachezaji ambao wanakupa kila unachokitaka kwa wakati sahihi wanapokuwa uwanjani.

Mfumo tata unaowachanganya wapinzani ambao anautumia kocha mkuu wa Yanga Miguel Gamond ni silaa nzito kwa El Merrikh kwa hakika mchezo unakwenda kumalizika huko huko Rwanda na mchezo wa pili ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa itakuwa ni kukamilisha ratiba tu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: