Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Al Hilal yamaliza kibabe Kagame

Al Hilal Kagameeeeeeee Al Hilal yamaliza kibabe Kagame

Sun, 21 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wababe wa soka wa Sudan, Al Hilal imemaliza michuano ya Kombe la Kagame 2024 iliyofikia tamati jana kwa kunyakua nafasi ya tatu kwa kuwafunga ndugu zao wa Al Wadi katika mchezo wa kuwania nafasi ya tatu uliopigwa kwenye Uwanja wa KMC, uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Al Hilal iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ya kubeba kwa mara ya kwanza taji la michuano hiyo, hasa baada ya Simba, Yanga na Azam kuchomoa kushiriki, ilipata nafasi hiyo kwa ushindi wa penalti 3-2 baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya bao 1-1, huku timu hiyo ikipoteza penalti mapema kipindi cha kwanza.

Pape Abdou alikosa penalti dakika ya 35 baada ya kipa wa Al Wadi kuucheza, lakini dakika nne baadae Altayeb Abakaer aliifungua Al Hilal bao la kuongoza.

Hata hivyo, bao hilo lilidumu kwa dakika tatu tu, kwani nahodha wa Al Wadi, Mohamed Adan alisawazisha na kufanya hadi mapumziko matokeo kuwa 1-1.

Kipindi cha pili licha ya timu zote kufanya mabadiliko na kupambana kusaka mabao mengine, lakini dakika 90 za pambano hilo lililopigwa kuanzia saa 6:00 mchana matokeo yalisalia kama ilivyo na timu hizo kupigiana penalti tofauti na ilivyokuwa katika nusu fainali zilichezwa kwa dakika 120 baada ya kuongezewa muda.

Kinara wa mabao wa michuano hiyo, Mohammed Abdelrahman aliyemaliza akiwa na mabao matano, ndiye aliyeihakikishia Al Hilal inayonolewa na kocha Florent Ibenge kwa kufunga penalti ya ushindi baada ya awali timu hiyo kupoteza mbili na Al Wadi ikapoteza ya mwisho.

Kwa matokeo hayo, Al Hilal imetwaa Dola 10,000 zaidi ya Sh 26 Milioni, fedha zinazotolewa na mdhamini mkuu wa michuano hiyo iliyoasisiwa mwaka 1967, Rais wa Rwanda, Paul Kagome aliyeziweka tangu 2002.

Chanzo: Mwanaspoti