Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Al Hilal yaikacha Ligi Kuu Tanzania

Al Hilal Omduran Sudan.jpeg Al Hilal yaikacha Ligi Kuu Tanzania

Fri, 24 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mujibu wa Mwandishi Nguli, Lassana Camara klabu mbili za Sudan Hilal na Merreikh zimekubaliana na mamlaka za soka na kinchi nchini Mauritania ili miamba hiyo ishiriki kwenye Ligi yao kutokana na vita inayoendelea nchini Sudan.

Mfumo ni kuwa timu zitashindana kama kawaida na bingwa atapatikana kwa wote ila kushiriki kimataifa hakuna kitakachoathirika ambapo timu ya kwanza kwenye msimamo kutoka Mauritania itacheza Champions League huku timu ya kwanza ya Sudan kwenye msimamo pia itacheza Champions League.

Wameshatuma maombi yao rasmi CAF na wanasubiri mrejesho kutoka Cairo, kwa maana hiyo Al Hilal kuja kucheza Tanzania imeota mbawa rasmi.

Klabu za Al hilal na El Merreikh za nchini Sudan zimekubaliwa ombi la kujiunga na ligi kuu Mauritania kwa ajili ya msimu ujao.

Hapo awali Al hilal ilituma ombi kwenye shirikisho la mpira wa miguu Tanzania [TFF] kutaka kujiunga na ligi ya Tanzania kuanzia msimu ujao ambapo TFF kupita bodi ya ligi walikubali ombi hilo kwa kanuni maalumu.

Wamebadili uamizi wao kwa sababu katika ligi ya Mauritania points watakazopata ligi kuu zitahesabiwa, wakitwaa Ubingwa watapata kombe na posho kama ambavyo timu za Mauritania zitapata.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live