Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Al Hilal yafuzu, sasa kukutana na Yanga

Al Hilal St George Gh Al Hilal yafuzu, sasa kukutana na Yanga

Sun, 18 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Miamba ya Soka ya Sudan Kaskazini, Al Hilal Obdurman imefanikiwa kusonga mbele katika hatua ya pili ya mtoani kombe la klabu Bingwa Barani Afrika baada ya kuwachapa mabingwa wa Ligi Kuu ya Ethiopia, St George kwa bao 1-0.

Al Hilal amefuzu kwa kanuni ya bao la ugenini ambapo mechi ya awali wakiwa ugenini walifungwa bao 2-1, hivyo kwa ushindi wa leo jumla ya matokeo ni bao 2-2 wakiwa na faida ya bao 1 la ugenini wakati St. George wakiwa hawana bao la ugenini.

Rasmi sasa Yanga Sc atacheza na vijana wa Frolent Ibenge, Al Hilal ambayo iliwahi kufundishwa na kocha Nasreddine Mohammed Nabi.

Ikumbukwe pia kwamba Ibenge amewahi kuwafundisha Fiston Mayele, Djuma Shaban, Tusila Kisinda, Joyce Lomalisa, Yanick Bangala wakati wakiwa AS Vita Club ya Congo DR.

Tutegemee soka la aina gani kati ya miamba hawa?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live