Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Al-Hilal kumng’oa Alejandro Garnacho Old Trafford

Alejandro Garnacho Likes Al-Hilal kumng’oa Alejandro Garnacho Old Trafford

Fri, 28 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MATAJIRI kutoka Saudia Arabia, Al-Hilal wameripotiwa kutuma maombi kwenda Manchester United ya kutaka kumsajili winga wa timu hiyo na Argentina, Alejandro Garnacho ambaye kwa sasa yupo katika michuano ya Copa America.

Taarifa za awali zinadai Al Hilal imewasilisha ofa nono, lakini Man United haina mpango wa kumuuza staa huyo kwa sasa.

ARSENAL huenda ikaambulia patupu katika mchakato wa kuiwania saini ya straika wa Stuttgart, Serhou Guirassy katika dirisha hili kutokana na kile kinachoelezwa kwamba staa huyu yupo katika hatua za mwisho kujiunga na Borussia Dortmund.

Serhou mwenye umri wa miaka 28, ni mmoja kati ya mastaa walioonyesha kiwango bora kwa msimu uliopita ambapo alifunga mabao 30 katika mechi 30 za michuano yote.

KOCHA wa Napoli, Antonio Conte amethibitisha kuwa anahitaji huduma ya straika wa Chelsea ambaye msimu uliopita alicheza kwa mkopo AS Roma, Romelu Lukaku.

Taarifa za awali zinaeleza Napoli inamwangalia Lukaku kama mbadala sahihi wa Victor Osimhen ambaye anadaiwa huenda akaondoka katika dirisha hili. Msimu uliopita Lukaku alicheza mechi 50, akafunga mabao 21.

RAIS wa Napoli, Aurelio De Laurentiis amesisitiza kuwa hana bifu lolote na winga wa timu hiyo Khvicha Kvaratskhelia lakini hatouzwa kwenda popote.

Hivi karibuni iliibuka sintofahamu baada ya Lauirentiis kusema winga huyo hauzwi halafu baadaye wakala wa Khvicha akaibuka na kusema mchezaji wake anataka kuondoka, jambo lililoashiria msuguano kati ya pande mbili hizo.

Paris Saint-Germain ni miongoni mwa timu zilizoonyesha nia ya kutaka kumsajili.

WAKALA wa Lautaro Martinez amesisitiza kwamba mchezaji wake hatoenda popote katika dirisha hili la majira ya kiangazi licha ya tetesi kudai kwamba huenda akauzwa.

Martinez ambaye mkataba wake na Inter Milan unamalizika mwaka 2026, alionyesha kiwango bora katika Serie A akiwa na timu hiyo kwa msimu ulipopita ambapo alifunga mabao 27 na kuibuka mfungaji bora wa ligi.

MANCHESTER United imeingia kwenye vita ya Aston Villa na Chelsea ya kuiwania saini ya mshambuliaji wa Hoffenheim, Maximilian Beier, 21, katika dirisha hili.

Beier ambaye msimu uliopita alicheza mechi 36 za michuano yote na kufunga mabao 16, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.

ARSENAL imefikia patamu katika harakati za kuiwania saini ya kiungo wa Real Sociedad, Mikel Merino katika dirisha hili baada ya kuvutiwa na kiwango bora alichoonyesha akiwa na Sociedad na timu ya taifa ya Hispania katika michuano ya Euro mwaka huu. Inaelezwa Mikel Arteta ndio anasimamia mchongo mzima wa kutaka kumsajili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live