Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Al Hilal kucheza Ligi Kuu ya NBC

Al Hilal Omduran Sudan.jpeg Al Hilal kucheza Ligi Kuu ya NBC

Mon, 18 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Al Hilal ya Sudan imewasilisha barua kwa Mashirikisho ya soka ya nchi mbalimbali ikiwepo Tanzania kuomba kushiriki ligi kwa ajili ya kuwa kwenye ushindani.

Hilo linakuja kipindi hichi baada ya ligi ya Sudan kusimama kwa sababu za kiusalama baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe huku Hilal wakihitaji mechi za ushindani kwa ajili ya kuwa timamu

Moja kati ya mashirikisho yaliyopokea barua hizo ni pamoja na shirikisho la soka Tanzania (TFF) ambapo kwa mujibu wa mwandishi wa habari za michezo barani Afrika Micky Jr, TFF imerdhia ombi hilo na kwasasa wapo kwenye hatua za mwisho za kikanuni kuangalia kama inawezekana kwa vigogo hao wa soka ukanda wa CECAFA kuja kushiriki ligi kuu Tanzania bara na kama kanuni zitaruhusu basi tutawashuhudia Al Hilal nchini.

Pia moja kati ya sababu zinazoweza kusaidia hilo kupita ni uhusiano mzuri kati ya Al Hilal na TFF pamoja na klabu kubwa za Tanzania yaani Simba na Yanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live