Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Al Ahly yalazimishwa sare nyumbani

Al Ahly Yalazimishwa Sare Nyumbani.jpeg Al Ahly yalazimishwa sare nyumbani

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya soka ya nchini Misri, Al Ahly, imelazimishwa sare ya 0-0 dhidi ya Smouha wakiwa nyumbani.

Wapinzani hao wa Al Ahly, wapo nafasi ya 9 kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini Misri huku Al Ahly wakiwa nafasi ya pili chini ya Pyramids.

Al Ahly, wanatarajiwa kushuka dimbani Jumamosi hii Desmba 2, 2023 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar mechi ya pili ya hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa Afrika.

Mchezo wao wa kwanza, Al Ahly alitoka kifua mbele kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Medeama huku Yanga akiambulia kichapo cha 3-0 kutoka kwa CR Belouizdad.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live