Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Al Ahly yaizamisha Medeama

Ahly Shangwe Al Ahly yaizamisha Medeama

Sat, 24 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Al Ahly leo imefifisha matumaini ya Medeama kutinga hatua ya 8 bora Klabu Bingwa Afrika baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu hiyo ya Ghana.

Bao hilo la Al Ahly kwenye mchezo huo wa kundi D uliofanyika uwanja wa michezo wa Baba Yara, Kumasi Ghana limefungwa na Hussein El Shahat katika dakika ya 48.

Al Ahly imefikia pointi 9 baada ya michezo 5 wakati Medeama imebaki na pointi 4.

Katika mchezo mwingine wa kundi hilo Februari 24 Yanga yenye pointi 5 itashuka dimba la Benjamin Mkapa kuikabili CR Belouizdad ya Algeria pia yenye pointi 5.(Picha:Al Ahly SC)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live