Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Al Ahly yaanza kubeba mataji

Ahly Ubingwa Al Ahly yaanza kubeba mataji

Sat, 9 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati ikisikilizia droo ya merchi za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ndio watetezi wa taji, Al Ahly ya Misri imeanza kukusanya mataji ya msimu huu baada ya jana usiku kuwafumua wapinzani wao, Zamalek katika mechi ya kuwani Kombe la Misri (Egypt Cup).

Hilo ni taji la kwanza kwa timu hiyo msimu huu baada ya awali kushindwa kutwaa CAF Super Cup mbele ya USM Alger ya Algeria na lile la African Football League (AFL) ilipokwamia hatua ya nusu fainali kwa kutolewa na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini iliyoibuka mabingwa wa kwanza wa michuano hiyo mipya barani humu.

Mabingwa hao wa kihistoria wa Afrika na klabu inayoshirikilia rekodi ya klabu yenye mataji mengi Afrika na duniani ikiizidi hdio Real Madrid, ilitwaa taji hilo kwa ushindi wa mabao 2-0 yaliyopatikana katika fainali iliyoamuliwa na mabao ya dakika za jioni dhidi ya Zamalek.

Bao la kwanza liliwekwa kimiani na Emam Ashour dakika ya 84 kisha Mohamed Magdy akaongeza la nyongeza na kuwata wababe hao wa Misri taji la 40 la michuano hiyo.

Hilo linakuwa ni taji la kwanza kuchukuliwa na Ahly tangu kuanza kwa mwaka huyu tena mbele ya mahasimu wao Zamalek.

Ahly inaonekana kuwa na kiwango bora kwenye Ligi Kuu ambapo inashika nafasi ya 10 ikiwa na viporo vya mechi nane ambazo ikishinda zote itafikisha pointi 31 na kuishusha ENPPI ambao ndio vinara kwa sasa wakiwa na pointi 26 walizopata kwenye mechi 15, huku Ahly ikiwa imecheza mechi saba tu.

Hadi sasa Ahly ndio timu pekee ambayo haijapoteza mechi yoyote kwenye Ligi Kuu Misri ikiwa imeshinda mechi tano na kutoa sare mbili.

Al Ahly imetinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuongoza Kundi D mbele ya Yanga iliyomaliza ya pili baada ya kuzidi ujanja CR Belouizdad ya Algeria na Medeama ya Ghana na sasa zinataka kujua zitacheza na timu zipi mara baada ya droo itkayopangwa Jumatano ijayo (Machi 12).

Timu nyingine zilizotinga hatua hiyo ni Simba ya Tanzania, Mamelodi, Esperance ya Tunisia, Petro Atletico ya Angola, Asec Mimosas ya Ivory Coast na TP Mazembe ya DR Congo.

Chanzo: Mwanaspoti