Vigogo wa Afrika, Timu ya Al Ahly wamwfanikiwa kunyakuwa Ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa msimu wa mwaka 2022/2023 baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Bingwa mtetezi Wydad Casablanca mchezo katika mchezo wa Fainali ya Mkondo wa pili Jumapili usiku.
Mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Mohammed V uliwashuhudia Al Ahly wakijihakikishia Ubingwa kwa bao la dakika za jioni la kusawazisha la mlinzi Mohamed Abdelmonem akisawazisha bao la kuongoza la Wydad lililoffungwa na Attiyat Allah 27’.
Sare ya bao 1-1 ikawafanya Ahly kushinda kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2 baada ya kushinda mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Juma lililopita nchini Misri.
Ubingwa huo unawafanya Ahly kuweka rekodi ya kubeba taji la Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya 11, mara nyingi zaidi kuliko klabu yoyote.