Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Al Ahly uso kwa uso na Real Madrid

Al Ahly World Cup Al Ahly uso kwa uso na Real Madrid

Tue, 7 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

AL Ahly itamenyana na mabingwa wa kihistoria wa Ligi Mabingwa Ulaya, Real Madrid kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Dunia ngazi ya klabu.

Bao la dakika za lala salama lililowekwa nyavuni na Mohamed Afsha dakika ya 88 wikiendi iliyopita limeipeleka Al Ahly nusu fainali katika michuano hiyo inayochezwa Morocco.

Al Ahly iliifunga bao 1-0 Seattle Sounders kwenye Uwanja wa Tangier, lakini ina kibarua dhidi ya Madrid yenye historia ya kubeba kombe hilo mara nne.

Madrid ilijikuta katika wakati mgumu na kukubali kichapo cha bao 1-0 kwenye mechi ya La Liga ilipomenyana dhidi ya Mallorca wikiendi iliyopita.

Baada ya kipigo hicho Madrid imeachwa pointi nane na Barcelona kwenye msimamo wa La Liga baada ya ushindi wake wa mabao 3-0 dhidi ya Sevilla.

Madrid imesuasua katika mechi zake za hivi karibuni lakini Kocha Carlo Ancelotti amedai kikosi chake kina majeruhi wengi.

Katika mechi nyingine ya robo fainali Al Hilal kutoka Saudia Arabia iliifunga Wydad Athletic kwa penalti 5-3, timu hiyo itacheza nusu fainali ya kwanza leo dhidi ya Flamengo. Fainali ya Kombe la Dunia ngazi ya klabu itachezwa Februari 11 mwaka huu jijini Rabat, Morocco. Madrid inashiriki michuano hii mara sita 2014, 2016, 2017 na 2018. Chelsea ndio bingwa mtetezi wa kombe hili lakini ikashindwa kutetea ubingwa wake.

Fainali ya Kombe la Dunia ngazi ya klabu itachezwa Februari 11 mwaka huu jijini Rabat, Morocco. Madrid inashiriki michuano hii mara sita 2014, 2016, 2017 na 2018. Chelsea ndio bingwa mtetezi wa kombe hili lakini ikashindwa kutetea ubingwa wake.

Chanzo: Mwanaspoti