Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeitangaza rasmi Desemba 22, mwaka huu, kuwa ndiyo siku utakaochezwa mchezo wa Super Cup.
Mtanange huo utazikutanisha mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly, na Raja Casablanca ya Morocco ambayo ilitwaa taji la Kombe la Shirikisho.
Al Ahly waliitwaa ndoo ya Ligi ya Mabingwa kwa kuifunga Kaizer Chiefs mabao 3-0 katika mchezo wa fainali, wakati vigogo wa soka la Morocco, Raja, walitwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho kwa kuitandika JS Kabylie mabao 2-1.
Hata hivyo, Al Ahly ndiyo timu iliyotwaa mara nyingi ubingwa wa Super Cup ikiwa imelipeleka nchini Misri mara saba, ikiwamo mwaka jana kwa kuifunga RS Berkane.