Unamkumbuka Mac Muga? Sio yule msela wa Alikiba aliyepotea Afrika ya Kusini na kwenda kutoboa kimaisha, sio huyo. Huyu ni Mac Muga msela aliyevalia jezi nambari 10 mgongoni, ndio huyo Muga ninayemsemea mimi.
Ni yule Muga aliyetoka mitaa ya Msimbazi na kwenda mitaa ya Jangwani kusaka tonge lake. Ni yule Mac Muga ambaye na yeye pia kwa upande wake Mungu hakuwa Athumani ndani ya Jangwani.
Mac Muga alitusua Jangwani wakuu ambapo ulikuwepo ukame wa Burudani. Mac Muga alipewa jezi namba 10 ambayo wanapewa top players pekee ndani ya timu, lakini pia Mac Muga alipewa kitambaa cha unahodha, Mac Muga ulipendwa sana lakini ndio hivyo muda unakimbia sana.
Muga alituonesha Brazil ndani ya Tanzania, Muga alituonesha Ulaya ndani ya Afrika, that's was our magician Mac Muga.
Muga alitunyima imani ya utukufu tuliyompa ya "new Sammata in town", utukufu wetu wa upako tuliamini Muga angepita njia za Mbwana lakini Muga ulitunyima upako wa imani hiyo.
Katika kumbukumbu mbaya kwa Muga ni ile siku anahitajika na Klabu ya TP Mazembe ya nchini Congo, kipindi TP Mazembe ikiwa ni bora ndani ya Afrika, ikiwa inatazamwa na watu wengi.
Muga aliikataa TP Mazembe na kubakia Tanzania huku akirudi mitaa aliyokulia ya Msimbazi kugombania namba na The Bsest Triple C.
Kilichofuata ni historia kama ya Mac Muga wa Alikiba. Mitaa itamkumbuka Mac Muga, mwamba mwenye unyama wake anayejitafuta kwa Wanaume wa Tanga 'Waja leo Warudi leo'.