Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akon kusherehesha droo za AFCON

Akon To Perform AFCON Akon kusherehesha droo za AFCON

Thu, 12 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii mkubwa wa Afrika na dunia, Akon amechanguliwa kuwa mshehereshaji (MC) katika fainali ya upangwaji wa droo ya fainali za mataifa Afrika zitakazofanyika leo Oktoba 12, 2023 nchini Ivory Coast.

Droo hizo zitaanza saa 1:00 usiku kwa saa za Ivory Coast huku kwa Afrika Mashariki ikiwa ni saa 4:00 usiku.

Msanii huyo kutoka Senegal ni shabiki mkubwa wa soka na sasa yupo na mradi wake 'Akon Lighting Africa' ambao unahamasisha watu wa Afrika kutumia sola ili kutimiza majukumu yanayotaka umeme.

Akon atakuwa kwenye droo hizo ambazo zinatarajiwa kutizamwa na nchi takribani 50.

Mashindano hayo makubwa ambayo kwa sasa ni mara ya 34 yataanza kufanyika Ivory Coast Januari 13 hadi Februari 11, 2024.

Timu ambazo zitakuwa kwenye droo ni Ivory Coast, Algeria, Angola, Burkina Faso, Cameroon, Cape Verde, Congo DR, Egypt, Equatorial Guinea, Gambia na Ghana.

Nyingine ni Guinea, Guinea-Bissau, Mali, Mauritania, Morocco, Mozambique, Namibia, Nigeria, Senegal, South Africa, Tanzania, Tunisia and Zambia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live