Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akandanaho aikanda Simba na kuipa ubingwa Mlandege

Akandanaho Msks Akandanaho aikanda Simba

Sun, 14 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlandege ikionyesha kiwango cha hali ya juu imefanikiwa kuichapa Simba bao 1-0 na kutwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi.

Simba ikiwa kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, ilionyesha kiwango kizuri lakini safu ya ulinzi ya Mlandege ilikuwa imara muda wote.

Mlandege ilifanikiwa kujipatia bao pekee kupitia kwa kiungo mshambuliaji Joseph Akandanaho ambaye aliwachambua mabeki wa Simba na kufunga bao safi, liloifanya itetee ubingwa, ikiwa ni rekodi kwao.

Hata hivyo, Joseph alikuwa kama sapraizi kwa upande wa Simba kwa kuwa kwenye michezo mingine ya nyuma hakuwahi kuonekana kama ambavyo jana Simba ilimtumia, Ladack Chasambi.

Mwaka jana, Mlandege ilitwaa ubingwa huu baada ya kuichapa Singida mabao 2-1 na imeweka rekodi ya kuwa timu ya Zanzibar kutwaa ubingwa huo mara mbili.

Hii ilikuwa mechi ya kwanza kwa Mlandege kushinda ndani ya dakika tisini kwenye michuano hii msimu huu baada ya michezo yake yote kutoka sare na mingine kuingia kwa mikwaju ya penalti.

Katika mchezo wa jana, Simba ilikosa nafasi kadhaa kupitia kwa Fabrice Ngoma, Willy Esomba Onana na Jean Baleke huku, Mlandege ikianza kwa kukosa nafasi ya wazi dakika ya 17 baada ya kipa Ayoub Lakred kufanya makosa lakini ikashindwa kuitumia nafasi hiyo.

USHAMBULIAJI TATIZO SIMBA

Simba bado inatakiwa kuendelea kutafuta dawa ya safu ya ushambuliaji ambayo licha ya Kocha Abdelhak Benchikha kuwatumia washambuliaji wake wawili vinara Mosses Phiri na Jean Baleke wote wakicheza kipindi kimoja bado hawakuwa na kitu cha kuisaidia timu hiyo.

“Hayakuwa matarajio yetu, lakini tuseme ndiyo mpira ulivyo, tunawaomba mashabiki waendelee kutuunga mkono,” nahodha wa Simba Shomary Kapombe alisema.

ALIKIBA NDANI

Msanii Alikiba ndiye aliyekuwa msanii mkubwa aliyenogesha burudani kwenye mchezo huo huku wimbo wake wa Mnyama maalumu kwa Simba, ukiteka umati wa mashabiki wengi wa Simba wakiuimba Uwanja mzima.

RAIS KAMA KAWA

Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi kama kawaida ndiye aliyekuwa mgeni rasmi kwenye mchezo huo akitinga mapema tu dakika 25 kabla ya mchezo kuanza pia akiwemo makamu wake wa pili Hemed Suleiman na viongozi wengine wa serikali kwa Bara na Zanzibar.

TUZO

Mchezaji bora wa Mashindano: Fabice Ngoma (Simba) Kipa Bora wa Athuman Hassan (Mlandege). Mfungaji Bora: Elvis Rupia Singida Fountain Gate

Chanzo: www.tanzaniaweb.live