Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akaminko kuhusu Yanga: Niko tayari kwa lolote

AKAMINKO MORRISON Akaminko

Mon, 9 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya uongozi wa klabu ya Yanga kuuandikia barua uongozi wa Azam FC ili waweze kufanya mazungumzo kuhusa usajili wa nyota wawili wa Azam FC ambao ni James Akaminko na Kipre Junior katika dirisha hili dogo la usajili, Kisha Azam FC waliwajib Yanga kuwataka wasubiri mpaka mchezo kati ya Azam na Mbeya City umalizike na viongozi wa Azam FC wakae kujadili suala hilo.

Kwa mara ya kwanza James Akaminko ambae anahitajika na Yanga amefunguka kuhusiana na deal hili la juhitajika na Yanga

“Kwa sasa kila kitu kipo chini ya maboss wangu nasikiliza kile watakachokiamua maana kwa sasa bado nina mkataba nao (AZAM FC) siwezi kuchagua lolote hivyo nasubiri maamuzi yao.

Kama Azam wataamua nipo tayari kwa lolote, nipo tayari kwa ajili ya maisha yangu, kwa sasa mimi ni mchezaji wa Azam siwezi zungumza kuhusu Yanga,” James Akamiko kiungo wa Azam Fc.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live