Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akaminko anapatikana, Yanga wanasubiri nini?

James Akaminko Kazi James Akaminko.

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kushuhudia kiwango 'kibovu' kutoka kwa Zawadi Mauya (Jumapili iliyopita) kwenye mchezo wa Robo Fainali ya Michuano ya Mapinduzi Cup dhidi ya APR, na kushindwa kufikia malengo kwa, Jonas Mkude, Yanga SC wanapaswa kufanya usajili wa 'kushtukiza' na wa lazima, kumsaini, James Akaminko kutoka Azam FC.

Ndiyo, michezo minne ambayo Yanga wameicheza kwenye michuano ya Mapinduzi huko Visiwani Zanzibar, imeonyesha kuporomoka kwa viwango vya wachezaji wengi, na wakati huu wakiwa tayari wamefanikiwa kuwasaini, Shekhan Khamis na Mghana, Agustine Okrah, usajili wa Akaminko unaweza kuwa na umuhimu mkubwa kuliko nyongeza ya mshambulizi wa kati, japokuwa pia ni hitaji jingine ambalo timu inatakiwa kulikamilisha kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili, Januari 15.

Crispin Ngushi tayari ametimiza miaka miwili kikosini, Yanga tangu aliposajiliwa kutoka Mbeya Kwanza, Desemba, 2021, ni hivyo pia kwa Dennis Nkane Kipa, Abdultwalib Mshery ambao pia walisajiliwa katika dirisha dogo la usajili sambamba na Ngushi wakitokea vilabu vya Biashara United, na Mtibwa Sugar FC, kwa matarajio ya baadae lakini baada ya timu kuondolewa kwa kipigo kizito cha mabao 3-1 na APR, wachezaji hao wameshindwa kuthibitisha uwanjani kama wanaweza kufikia malengo hayo.

Ukichanganya na kuporomoka kwa viwango vya Mauya, Jesus Moloko, Farid Musa na kuendelea kucheza kwa kiwango cha chini kwa Mkude, na Mathlese Makudubela, na sistofahamu ya uwezo halisi wa Gift Fred moja kwa moja kunaondoa dhana ya kikosi kipana ambacho Yanga walitamba nacho msimu uliopita, kote, michuano ya ndani na kwenye mashindano ya CAF.

KWANINI, AKAMINKO SASA? Ni kwa sababu ataingia moja kwa moja kikosini na kusaidiana na Khalid Aucho. Ni muhimu sana, Yanga kumsaini kiungo huyo wa kati wa Azam FC hivi sasa kwa ssbabu, anapatikana na Azam FC wamekuwa wakizungumza na baadhi ya klabu za hapa nchini na nje ya nchi ili kumtoa kwa mkopo kupisha maingizo mapya ya wachezaji wa kigeni kikosini mwao.

Katika timu ya Azam FC, Akaminko anacheza sambamba na kina Sospeter Bajana, Yannick Bangala ambaye yupo kwenye kiwango bora kwa sasa.

Azam FC haina tatizo tena la uhaba wa kiungo wa ulinzi, eneo ambalo pia hucheza vizuri nahodha wa kikosi hicho, Mghana, Daniel Amoah , ndiyo maana wanamtoa Akaminko. Akija Yanga ataingia haraka kikosini na atatoa mchango wa moja kwa moja niamani.

Yanga watapata wakati mgumu sana endapo hawatashughulika kwa haraka na usajili wa kiungo wa ulinzi, kwa sababu Mauya, Mkude sio wa kuwategemea tena, na kwenda michezo 20 ya Ligi Kuu, Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la FA kwa kumtegemea, Aucho pekee litakuja pigo kwa klabu na timu itatema mataji yote inayoyashikilia ( Ligi kuu na FA). Lazima, Akaminko asajiliwe haraka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live