Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajiondoa Timu ya Taifa baada ya kuxiwa kufunga Ramadhani

Mahamadou Diawara (1).jpeg Mahamadou Diawara.

Sat, 23 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la soka Ufaransa (FFF) limewapiga marufuku wachezaji kufunga Ramadhan wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa.

Sheria mpya za FFF zinasema kwamba wachezaji walioitwa na timu za taifa za Ufaransa hawawezi kufunga kipindi cha Ramadhani wakati wakiwa na timu za Taifa.

Kila kocha mkuu wa timu za taifa za Ufaransa, kuanzia ngazi ya umri chini ya miaka 16 (U16), Lionel Rouxel hadi kocha mkuu wa timu ya wakubwa Didier Deschamps, waliwaambia wachezaji wao kuhusu Sheria hiyo mwanzoni mwa mapumziko ya kimataifa.

Nyota wa Olympique Lyon, Mahamadou Diawara ambaye aliitwa kwenye timu ya Taifa ya umri chini ya miaka 19 ya Ufaransa amelazimika kurudi nyumbani baada ya kubaini uwepo wa Sheria hiyo ambayo ingemlazimu kusimama kufunga kwa kipindi cha siku 8 za michuano ya Kimataifa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live