Nyota wa zamani wa Simba na Yanga anayekipiga Azam FC, Ibrahim Ajibu amesema bado kidogo tu wale waliokuwa wakimbeza wataanza kumpigia makofi.
Fundi huyo wa mpira alisema anaamini kupewa nafasi ya kucheza kila mara ndani ya timu hiyo mpya kwake, atafanya vizuri zaidi na kumsaidia kufikia malengo yake.
Akizungumza na Mwanaspoti, Ajibu alisema anaamini katika kila jambo Mungu yupo nyuma yake, hivyo atafanya makubwa akiwa na timu yake mpya kwa kushirikiana na wenzake.
“Namshukuru sana Mungu napata nafasi katika maisha yangu mapya, mimi kama mchezaji nafurahi na nafarijika kwa kuwa naonesha kitu kupitia wao walivyoniamini na kuniona nafaa kuwa katika timu yao,” alisema staa huyo aliyewahi kuwa nahodha wa Yanga.