Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajibu atangaza vita mpya

Ajib Namba (600 X 718) Ibrahim Ajib

Fri, 23 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kabla ya Singida Big Stars kucheza mchezo wa kwanza Kombe la Mapinduzi mjini Unguja dhidi ya KMKM Januari 2, mwakani, itakuwa imemtambulisha nyota wake mpya, Ibrahim Ajibu Migomba kutokea Azam FC.

Juzi Azam FC ilitoa taarifa ya kumuaga Ajibu na baadaye kuelezwa ametimkia Singida ambayo inafanya vizuri kwenye ligi.

Alipotafutwa Ajibu alisema kuna maisha mapya anakwenda kuyaanza kwenye eneo lingine baada ya kumalizana na Azam FC, aliyoishi nayo kwa msimu mmoja kwenye mazingira mazuri.

Alisema si vyema kuweka wazi timu yake mpya hadi hapo atakapotambulishwa ila huko anakwenda kuonyesha kuwa si mchezaji aliyeshuka ubora kama wengi wanavyosema katika maeneo mbalimbali.

Alisema siyo kama haoni au hasikii maneno kuhusu ubora wa maisha yake ya mpira na wengine wakiamini kama amefeli baada ya kushindwa kuongeza mkataba mpya Azam ila yote hayo yatakwenda kujibiwa na miguu yake.

“Namuomba Mungu anipe afya njema nataka kwenda kuonyesha mfano, siyo kama nilishindwa kucheza Azam FC kwa ajili ubora, binafsi sipendi kuongea bali nitakwenda kuonyesha vitendo,” alisema Ajibu na kuongeza;

“Maisha yangu kwa kiasi kikubwa yapo kwenye mpira nikuhakikishie kila ninalolifanya ni sahihi kwa hatma yangu kwa sasa na hapo baadaye nitakapoachana na soka.

“Kutokana na usajili wangu mpya ulivyo kuna kazi kubwa natakiwa kwenda kuifanya kwenye timu yangu mpya binafsi naamini hilo linawezekana kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu,” alisema

Ajibu msimu uliopita alijiunga na Azam Fc, katika dirisha dogo akitokea Simba baada ya kushindwa kupata nafasi ya kucheza huko kwenye misimu yote miwili akirejea hapo akitokea Yanga.

Akiwa na Yanga katika msimu wake wa pili, Ajibu alionekana kuwa kwenye kiwango bora chini ya Kocha Mwinyi Zahera baada ya kumaliza msimu akifunga mabao saba na kutoa pasi za mwisho 14, Simba ilivutiwa na huduma yake ilimrudisha kikosini.

Chanzo: Mwanaspoti