Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajibu asaini miwili Singida Big Stars

Ajibu Ibrahim Ibrahima Ajib

Wed, 21 Dec 2022 Chanzo: dar24.com

Siku moja baada ya kuagwa rasmi Azam FC, Kiungo Mshambuliaji Ibrahim Ajibu amekamilisha dili la kujiunga na Klabu ya Singida Big Stars, inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2022/23.

Kiungo huyo aaliyewahi kuzitumikia Simba SC na YoungA fricans kwa nyakati tofauti, amejiunga na Miamba hiyo ya Singida kwa mkataba wa miaka miwili, na wakati wowote anatarajiwa kuonekana kwenye kikosi cha kwanza cha Kocha Hans Van Der Pluijm.

Ajibu amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili akitokea Azam FC, baada ya kuelezwa aligoma kwenda Polisi Tanzania inayofundishwa na Kocha wa zamani wa Yanga, Mwinyi Zahera.

Ajibu ambaye ni zao la timu ya vijana ya Simba SC amekuwa akitajwa mara kwa mara kuwa miongoni mwa viungo bora zaidi Tanzania, ingawa hakupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Azam FC.

Chanzo: dar24.com