Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajibu apewa mchongo

Ajibu+pic Ajibu apewa mchongo

Wed, 19 Aug 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Imani MakongoroMshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu ameshauriwa kufikiria maisha ya kucheza soka la kulipwa nje ya nchi ili kupata changamoto mpya kisoka.

Ushauri huo umetolewa na aliyewahi kuwa mchezaji na kocha wa Simba kwa nyakati tofauti, Abdallah Kibadeni 'King'.

Kocha huyo alisema mchezaji huyo ana uwezo mkubwa kisoka, ingawa bado hajaamua kuutumia ipasavyo.

"Ajibu ana kiwango cha juu, hata kwa wachezaji wazawa wanaocheza nafasi sawa na yeye binafsi bado sijaona wa kumfunika, sema bado hajaamua kukitumia kipaji chake ipasavyo," alisema Kibadeni.

Alisema mchezaji huyu akifanikiwa kupambana na kujihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza cha Simba atakuwa ni habari nyingine.

"Hivi sasa ni kama amepooza, yale makeke yake ya soka yanapotea, lakini nafikiri anapewa presha na wachezaji wa kigeni, ila bado ana fursa ya kupambana na kutoka.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz