Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajibu amvuruga Gomes

Ajibu Pic Data Ajibu amvuruga Gomes

Mon, 1 Mar 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Thobias SebastianMore by this Author SOKA tamu lililojaa ufundi na umakini, lililopigwa na kiungo mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu limemvuruga kocha wake, Didier Gomes, huku nyota huyo akisisitiza akizidi kupewa nafasi kikosini atafanya mambo makubwa zaidi kuliko alichokifanya kwenye Kombe ASFC.

Wekundu wa Msimbazi hao juzi walishinda mabao 3-0 dhidi ya African Lyon na kutinga 16 Bora ya michuano hiyo ya ASFC, huku Ajibu akitupia mbili nyavuni na jingine likiwekwa kimiani na Perfect Chikwende na Kocha Gomes amemsifia sana Ajibu akidai ni bonge la fundi.

Akizungumza na Mwanaspoti juzi jijini Dar es Salaam, Gomes alisema Ajibu ameonyesha kiwango bora katika mechi hiyo ya ASFC na kwamba anaongeza ushindani zaidi wa namba kwenye nafasi anayocheza ili aingie kikosi cha kwanza alichodai pia kina wachezaji wengine wakali kama yeye.

Gomes alisema hana utamaduni wa kusifia mchezaji mmoja mmoja, lakini alichokifanya Ajibu kimemkuna kama alivyokuna na soka la wengine aliowaanzisha kwenye mchezo huo hasa wale wasiopata nafasi katika kikosi cha kwanza.

“Ajibu ni mchezaji mzuri mwenye uwezo wa kumiliki mpira, jicho la kupiga pasi yenye hatari, kufunga mabao pamoja na mambo mengine na alistahili kuonyesha kiwango hicho kwa vile alikuwa akikifanya hata mazoezini,” alisema Gomes na kuongeza;

“Niwapongeze wachezaji wangu hawakuonyesha utofauti mkubwa licha ya kubadilisha kikosi hii inaonyesha jinsi gani nao wanataka kupewa nafasi ya kutumika zaidi kwani wana viwango bora na malengo yetu ni kutetea kombe hili.”

Chanzo: mwanaspoti.co.tz