Winga Ibrahim Ajibu, ameanza mazungumzo mapya na Coastal Union, baada ya kumaliza mkataba wake wa mwanzo msimu ulioisha, wakati huo huo mkononi mwake akiwa na ofa za timu nyingine za Ligi Kuu.
Ukiachana na Coastal Union, timu nyingine zinazotajwa kumpelekea ofa Ajibu ni Namungo, KMC na Kagera Sugar na rafiki wa karibu wa mchezaji huyo, ameeleza anaangalia ni timu yenye maslahi mapana ili asaini.
Staa huyo wa zamani wa Yanga, Simba na Azam ni miongoni mwa wachezaji wenye uzoefun mkubwa kwenye Ligi hiyo na ndio sababu kubwa ya makocha mbalimbali kutaka kuwa nae kikosini.
Msimu uliopita alichangia kwa kiasi kikubwa kikosi hicho kunasa kwenye nafasi ya nne na wana mipango nae msimu ujao kwenye michuano ya kimataifa ambayo alishashiriki akiwa na timu maarufu za Dar es Salaam.