Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajibu, Manula wabakishwa Dar

69553 Manula+picha

Sat, 3 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

TIMU ya Taifa, Taifa Stars ambayo muda huu inajiandaa kupaa kwenda Kenya, itaondoka bila baadhi ya nyota wake akiwamo kipa Aishi Manula, beki David Mwantika na kiungo mshambuliaji Ibrahimu Ajibu walio na matatizo mbalimbali ikiwamo majeruhi.

Stars inaondoka jioni  hii kwenda Nairobi, Kenya kwenye  mchezo wa marudiano wa Mabingwa wa Mataifa ya Afrika (Chan) dhidi ya Kenya, Harambee Stars.

Timu hiyo inatarajia kuondoka bila beki Aishi Manula, David Mwantika ambao ni majeruhi.

Pia katika orodha, wachezaji waliyokosekana ni Ibrahim Ajibu ambaye ndiye alikuwa wa kwanza kuondolewa katika kikosi cha timu hiyo.

Mratibu wa Timu ya Taifa Stars, Danny Msangi alisema kwamba tayari wamejipanga vilivyo katika kuziba pengo la wachezaji hao wawili (Manula na Mwantika).

Wakati huo huo; Nahodha wa Taifa Stars, Erasto Nyoni alisema,” Taifa Stars lazima ipambane ili kulinda heshima ya nchi”.

Pia Soma

"Watanzania wanapenda timu ya mpira wa miguu ya taifa na hii lazima ituchochee kufanya vizuri zaidi kuliko kwenye mzunguko wa kwanza."

Nyoni alisema wanajua kuwa watakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Harambee Stars, lakini wamefunza kusudi la ushindi kushinda.

Timu hiyo ilitoka droo katika mechi ya kwanza iliyofanyika jijini Dar es salaam Jumapili.

Chanzo: mwananchi.co.tz