Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aizi Ki atua Bongo, muda wowote aananikwa Jangwani

Aziz Ki Katua Stephen Aizi Ki

Thu, 14 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afisa Habari wa Klabu ya Yanga Hassan Bumbuli amethibitisha kuwa mchezaji Stephen Aziz Ki tayari ameshatua nchini Tanzania kwa ajili ya kutambulishwa kama mchezaji mpya wa klabu hiyo.

Akiongea na chombo kimoja cha habari nchini leo asubuhi Bumbuli ametoa tamko hilo kufuatia kiu ya mashabiki wa timu ya Wananchi ambao walitarajia mchezaji huyo angeweza kutambulishwa jana usiku.

Bumbuli amesema Aziz Ki alikwisha malizana na Yanga tangu muda mrefu kilichokuwa kinasubiriwa ni yeye kumalizia msimu akiwa na klabu yake aliyokuwa akiichezea msimu uliopita ya Asec Mimosas ya nchini Ivory Coast.

“Aziz Ki ni mwananchi kwa asilimia 100 nduguyangu wana Yanga wasiwe na wasiwasi, sema watu wanasahau haraka sana na sijui kwanini wanasahau au sijui waandishi mnawasahaulisha!

"Tulishatoa taarifa mapema mara baada ya Rais Injini Hersi kwenda kumalizana naye kule tulithibitisha kuwa ni mwananchi na ameshasaini kandarasi ya kuitumikia Yanga.” Amesema Bumbuli

Klabu ya Yanga hadi sasa imekwisha kamilisha dili za usajili wa wachezaji wanne wa kigeni akiwemo Lazarous Kambole, Bernard Morrison, Gael Bigirimana pamoja na Joyce Lomalisa Mutambala huku usajili wa Aziz Ki ukisubiriwa kwa hamu miongoni mwa mashabiki wengi wa klabu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live