Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aishi Manula kama Harry Maguire tu!

Manula Maguire Aishi Manula kama Harry Maguire

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia EA Radio, Justine Kessy amesema kuwa kipa wa Simba SC, Aishi Manula ameporomoka kiwango kwenye timu yake na amekuwa haisaidii badala ya kuinyima matokeo.

Kessy amesema hayo baada ya Manula kuonesha kiwango duni kwenye mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons uliomalizika kwa Simba kupokea kichapo cha bao 2-1 huku akimfananisha Manula na Harry Maguire, beki wa kati wa Manchester United.

“Manula sasa hivi namuona kama Harry Maguire. Maguire linapokuja suala Timu ya Taifa ya Uingereza anakuwa hodari na mahiri kweli kuisaidia timu yake ya taifa, lakini akienda Manchester United anafanya vitu vya hovyo, form yake inakuwa mbaya.

“Manula alivyokwenda AFCON tukaanza kujiuliza, kwamba Ayoub atakaa benchi na nani atakuwa kipa namba mbili, Ally Salum au Ayoub. Sasa hivi tunaona akicheza Manula, Simba wanavyopata shida lakini akidaka Ayoub anafanya vizuri.

“Mimi ninaamini kwa sasa Ayoub ndiye kipa anayestahili kukaa kwenye milingoti mitatu ya Simba SC hasa kwenye mechi za Kimataifa lakini manula ataenda kutia aibu, atubiri kidogo. Manula asubiri timu ya Taifa kwa sababu hatuna kipa mwenye daraja lake.

“Manula kwa sasa anaogopa kujirusha kwa sababu anaweza kutonesha tena sehemu alipofanyiwa upasuaji kwa sababu akiumia akakaa nje mwaka mmoja tena ndiyo bye bye,” amesema Justine Kessy.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live