Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aisha Mnuka, 'Queen' wa hattrick Ligi Kuu ya wanawake

Aisha Mnuka Aisha Mnuka.

Wed, 17 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Simba Queens, Aisha Mnuka hivi sasa amefikisha hat-trick mbili katika Ligi Kuu ya Wanawake inayoendela huku akifunga mabao nane.

Aisha ametupia hat-trick ya pili katika mchezo dhidi ya Amani Queens uwanja wa Ilulu, Lindi ambapo Simba Queens imeshinda mabao 3-2.

Licha ya kuwa na hat-trick nyingi Aisha anaungana na Stumau Abdalah wa JKT Queens na kuongoza safu ya ufungaji bora wa ligi hiyo wakiwa na mabao 8 Wakati Simba Queens akishinda ugenini.

Yanga Princens amepoteza mchezo wa mzunguko wa tano katika uwanja wa nyumbani (Azam Complex) dhidi ya Ceasiaa Queens kwa kukubali kipigo cha bao 1-0, huu unakuwa mchezo wa pili kupoteza na wa kwanza ilikuwa dhidi ya watani zao Simba Queens kwa mabao 3-1

Dabi ya Kanda ya kati Baobab Queens na Fountain Gate mchezo uliochezwa katika uwanja wa Jamuhuri Dodoma mchezo umeisha kwa sare ya mabao 2-2.

Mchezo mwingine uliyochezwa ni Geita Queens dhidi ya Bunda Queens mchezo uliomalizika kwa Bunda Queens kushinda mabao 2-0.

Katika msimamo wa Ligi, JKT Queens anaongoza kwa pointi 12 akicheza michezo minne, Simba nafasi ya pili pointi 12 michezo minne, Yanga Princess nafasi ya tatu na point tisa kwenye michezo tano, Geita Queens anaendelea kuburuza mkia nafasi ya 10 na akicheza mechi tano bila kupata pointi yeyote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live