Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aisha Masaka kuivaa Real Madrid

Aisha Masaka 18 Aisha Masaka kuivaa Real Madrid

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada yakuweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi ya Mabingwa ya Ulaya kwa nyota wa kike walipoinyoosha Paris FC kwa mabao 2-1, Aisha Masaka anayekipiga BK Häcken ya Sweden leo atakuwa na kibarua kingine mbele ya Real Madrid wakapoumana kwenye mfululizo wa mechi za ligi hiyo.

Aisha na wenzake watakuwa nyumbani kuwakaribisha wababe hao wa Hispania kwenye Uwanja wa Bravida uliopo mji wa Gothenburg, huku wakiwa ndio vinara wa Kundi D baada ya kushinda mechi ya kwanza iliyopigwa Ufaransa, japo nyota huyo wa Tanzania kutofunga bao kwenye mchezo huo.

Katika mechi iliyopita Aisha alianza kikosi cha kwanza na leo pia anaweza kuliamsha kutokana na kuendelea kuwa mchezaji muhimu kikosini tangu ajiunge nao msimu uliopita.

Timu ya Hacken inahitaji ushindi ili kujiweka pazuri kwani Chelsea inayowafukiza nafasi ya pili kwenye Kundui D itapepetana na Paris kwenye mechi nyingine ya kundi hilo. Hadi sasa mshambuliaji huyo wa Tanzania katika mechi 12 alizocheza amefanikiwa kuweka nyavuni mabao matano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live