Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aisha Masaka aandika rekodi mpya Ulaya

Aisha Masaka Rekodi Aisha Masaka aandika rekodi mpya Ulaya

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aisha Masaka anakuwa Mtanzania wa kwanza kucheza mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa wanawake wakati timu yake ya BK Hacken ilipokabiliana na na Paris FC huko Ufaransa jana usiku na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1

Hadi sasa, hakuna mwanasoka wa kike wa Tanzania ambaye amewahi kushiriki mashindano hayo na Masaka jana ameanza kikosi cha kwanza, amekuwa Mtanzania wa kwanza kufanya hivyo.

Mchezaji huyo anayeitumikia timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania 'Twiga Stars' ni miongoni mwa nyota walioanza katika kikosi cha BK Hacken katika mechi hiyo ya kundi D.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Masaka aliandika kuwa kusubiri kumekwisha akimaanisha yuko tayari kwa mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kana kwamba haitoshi, watu mbalimbali wameonekana kutuma jumbe za kumtakia kheri mchezaji huyo akiwemo Clara Luvanga aliyewahi kucheza naye pamoja katika kikosi cha Yanga Princess.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live