Menaja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally ametupa dongo kwa wapinzani wao, Yanga Sc baada ya kuwafunga na kuchukua Ngao ya Jamii Jumapili iliyopita katika Dimba la Mkwakwani Tanga.
Ahmed amesema viongozi wa Yanga waliona aibu wakakimbia hata kwenye tukio la kuvalishwa medali hawakuonekana huku wachezaji wao wakiwapandisha basi la RATCO badala ya kupanda basi lao la Yanga walilokwenda nalo Tanga.
Mchezo huo uliopigwa Jumapili Agosti 13, 2023 ulimalizika kwa sare hivyo ukaenda kwenye changamoto ya miukwaju ya penati ambapo Simba alifanikiwa kushinda kwa penati 3-1 na kubeba ubingwa huo.
"Wanajifariji heti wamecheza vizuri wakati wao na sisi on target moja moja, huo mpira mzuri wa kubutua nje umetoka wapi.
"Enhee baada ya kucheza vizuri mmepata nini? Maana viongozi wenu wamekimbia kuvaa Medali kwa kuona aibu mpira ni ubingwa, maonesho peleka Nanenane.
"Halafu imekuaje wenzetu mmerudi Dar na RATCO mmeona aibu kupanda basi lenu msizomewee? Hamu yetu na nyie haijaisha tukutane Novemba," amesema Ahmed Ally.