Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed akumbushia Simba ilivyonusurika kushuka daraja 1989

Ahmed Ally Xxx Ahmed akumbushia Simba ilivyonusurika kushuka daraja 1989

Wed, 29 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema si vibaya kwa Wana-Simba kujikumbusha kukumbukumbu mbaya lakini wakati mwingine ni vyema kufanya hivyo kwani zinafundisha.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ahmed ameandika hivi:

Haipendezi kujivunia mifano mibaya lakini, tunaitumia mifano hiyo kujikumbusha wapi tulipotoka. Mwaka 1989 Simba Sports tulinusurika kushuka daraja, kihistoria huo ndio msimu mbaya zaidi katika maisha yetu.

Binfasi nilikua na Miaka miwili lakini nilisikia uchungu kuona chama langu limepigania kushuka daraja na mbaya zaidi, Nyuma mwiko alikua bingwa maumivu makali iliyoje.

Msimu uliofuata yaani 1990 Simba tukachukua ubingwa wa Tanzania. Tazama hadithi hii ya kufurahisha, kunusurika kushuka daraja hadi kuchukua ubingwa ndani ya kipindi kifupi, rekodi hii duniani anayo Mnyama pekee.

Nini kilifanyika, Kwanza Wana Simba walikaa kwa utulivu, wakainisha mapungufu yao, wakaboresha madhaifu yao na wakaungana kwa misingi ya nguvu moja hatimae tukarejea katika ufalme wetu kwa haraka.

Mfano huu unatukumbusha kizazi chetu kuwa si ajabu timu kuporomoka na mfano huu unawakumbusha Vijana wa leo kuwa kuwa tumeshapitia mapito magumu zaidi lakini tulisimama imara.

Hatuna sababu ya kumtafuta mchawi, Utulivu na subira ndio jambo la msingi zaidi kujikwamua kwenye mkwamo huu.

Tuangalie namna gani tunaweza kuboresha timu yetu na hatimae turejee kwenye utawala wetu

Chanzo: www.tanzaniaweb.live