Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed aipiga dongo Yanga kwa Okrah

Okrah Amevunjika Pua Augustine Okrah

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Kabu ya Simba, Ahmed Ally amewatupia dongo watani zao, Yanga SC kuwa wamekuwa wakisajili wachezaji magarasa wanaotemwa na Simba.

Ahmed amesema kuwa, ni kawaida ya timu ndogo kama Yanga kusajili wachezaji waliotemwa na timu kubwa.

"Kila mchezaji anaeachwa ndani ya Klabu ya Simba kwa kushindwa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza, wenzetu wanamchukua.

"Hii inadhihirisha kuwa ndugu zetu wanaamini wachezaji wetu ni wazuri kuliko wao, na nikawaida mchezaji alieachwa na timu kubwa kusajiliwa katika timu ndogo," amesema Ahmed.

Ikumbukwe kuwa, hivi karibuni Yanga walimsajili kiungo Augustine Okrah (30) kutoka Ghana ikiwa miezi sita tu tangu aachane na watani wao, Simba SC.

Mwanzoni mwa msimu huu, Yanga walimsajili kiungo mzawa Jonas Mkude baada ya kuachwa na Simba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live