Klabu ya Simba imesema kuwa watani wao wa jadi yanga wamemchukua aliyekuwa kiungo wao mkongwe, Jonas Gerard Mkude baada ya klabu hiyo kuachana naye kutokana na sababu za kiufundi.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Kalbu ya Simba, Ahmed Allly wakati akihojiwa na chombo kimoja cha habari nchini kufuatia mchezaji huyo kutemwa na uongozi wa klabu yake huku akitajwa kuibukia Yanga.
“Kinachofanyika kwa Yanga wanatengeneza mazingira ionekane kama wametunyang’anya Jonas Mkude, au wametupiga bao hivi, ukweli utabaki kwamba wamechukua mchezaji ambaye Simba tumemuacha, na hivyo imekuwa ni utamaduni wao kwa miaka yote.
“Tulimuacha Bernard Morrison wakamchukua, tuemuacha Jonas Mkude wamemchukua kwa hiyo wao level yao ndiyo hiyo.
“Kama Simba tungemhitaji Mkude angebaki, hata yeye maisha yake ni Simba, hata kwa mkopo angebaki. Simba hii yenye neema asingekataa kubaki. Mkude ameishi kwenye Simba ngumu kweli, signing fee tunachangishanyana wakati Yanga wakiwa na Manji na pesa za kutosha.
“Sababu za kiufundi ndio zimesababisha Simba kuachana na Mkude, tungependa kuendelea kubaki naye lakini Simba ni timu ya kiushindani, watu wanataka matokeo makubwa, ni vigumu kubaki na mchezaji ambaye unaona kiufundi hatokuja kuwasaidia.
“Mkude hajashuka kiwango na si mchezaji mbaya, huko nakaokwenda anaenda kuwa top profile class player, wa kwao hawajacheza hata makundi ya Ligi ya Mabingwa, kwao wamelamba dume, atawasaidia pakubwa kweli. Simba tumatakia kila la kheri huko aendako.
“Siku ya Simba Day tutamuaga yeye ne Erasto Nyoni, wamefanya makubwa ndani ya Simba kwa hiyo hatuwezi kuwaacha wakaondoka hivi hivi. Hata kama timu yake Mkude itakataa, sisi kama Simba tutatimiza wajibu wetu hata kusimama na kumpigia makofi,” amesema Ahmed.