Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally kuanika majina ya wachezaji wote wanaotemwa

Ushindi Wowote Tunafuzu Hata Wa Goli Moja   Ahmed Ally Ahmed Ally.

Wed, 15 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja Habari na Mawasiliano Simba SC, Ahmed Ally amesema kuwa baada ya kutamatika tu, wataanza mchakato wa usajili mpya huku akisema kuwa wataanika majina ya wachezaji wote wanaotemwa.

Simba inapambana kumaliza katika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi ili msimu ujao iwe na nafasi ya kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

“Ingawa tunatarajia kufanya usajili mkubwa mara tu Ligi Kuu msimu huu itakapomalizika, lakini kwa sasa siyo wakati wa kuzungumzia chochote kuhusu hilo.

“Kwa sasa bado tupo kwenye ligi, hatuzuii tetesi za usajili, lakini ukweli wa kila kitu utabainika pale ligi itakapomalizika, nani atatoka na nani ataingia Simba SC, ila ukweli kwamba tunataka kufanya usajili mkubwa,” amesema Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live