Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally awatuliza mashabiki Simba kuchezea uwanja wa Meja Jeneral Isamuhyo

Ahmed Ally: Twendeni Uwanjani Hata Kama Tuna Hasira.jpeg Ahmed Ally awatuliza mashabiki Simba kuchezea uwanja wa Meja Jeneral Isamuhyo

Thu, 15 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba Ahmed Ally, amesema wana Simba hawapaswi kuwa na wasiwasi wowote kuelekea mchezo wa wa leo wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania.

Mtanange huo umekuwa gumzo mitandaoni kufuatia taarifa iliyotolewa na bodi ya ligi kuwa mchezo huo utapigwa Uwanja wa Meja Jeneral Isamuhyo na si Uwanja wa Azam Complex kama ilivyoelezwa awali wengi wakihoji uwezo wa uwanja huo kuandaa mchezo huo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ahmed ameandika.

"Nimeona wengi tumepanic baada ya kuona mechi yetu itachezwa Uwanja wa Meja Jeneral Isamuhyo, wengi tunaamini uwanja hauna vigezo vya kuchezea mechi kubwa na kuchezea timu kubwa.

"Kwanza kabisa tunapaswa kuheshimu mamlaka ambazo zimeupa Uwanja huo kibali. Pili tunapaswa kuwapongeza JKT Tanzania kwa uwekezaji waliofanya, JKT wamejenga Uwanja ili uchezewe mechi hivyo wanapopata kibali cha kutumia Uwanja wao ni faraja na mafanikio kwao," ameandika Ahmed Ally na kuongeza.

"Jambo la umuhimu kwetu ni kujikita na mchezo husika ili tuvune alama tatu

Hatupaswi kuwaza kuhusu uwanja, Sisi ni kwenda uwanjani kwa wingi na kuishangilia timu yetu ili tupate ushindi

Uwanja wa JKT hauna tofauti sana na Uwanja wa Manungu lakini, mwanzoni mwa msimu huu tulienda Manungu na kupata ushindi mnono

Ikumbukwe Simba wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na alama 33 katika nafasi ya pili baada ya michezo 14 huku JKT Tanzania wakiwa nafasi ya 12 na alama 16.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live