Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally awatolea uvivu wachambuzi, awapa neno hili!

Ahmed Ally 343 Ahmed Ally awatolea uvivu wachambuzi, awapa neno hili!

Wed, 8 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Jana kufanikiwa kuibuka na alama tatu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa hatua ya Makundi wakiichapa Vipers FC bao 1-0.

Wachambuzi wengi wa soka nchini wameonekana kutofurahishwa na kiwango cha Simba kinachooneshwa na Simba katika michezo yake msimu huu huku wengi wakisema sio Simba wanayoifahamu.

Sasa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ujumbe ambao unaonekana kuwalenga wachambuzi.

Ahmed ameandika;

"Ukisikiliza Radio unaweza kujua Simba ndo imefungwa jana, halafu ukisiliza tena unaweza kudhani Simba ndo ina point moja kwenye kundi letu, halafu ukitega sikio vizuri unaweza kuhisi kwamba Simba hakuna kitu kizuri tumefanya jana

Ila sisi ndo tunapenda mtukosoe hadi tufike Nusu Fainali tuliyokusudia".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live