Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally awatetea mastraika Simba

Ahmed Ally Awatetea Mastraika Simba .jpeg Ahmed Ally awatetea mastraika Simba

Tue, 20 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika orodha ya wafungaji 10 Bora kwenye michuano ya AFCON iliyomalizika Nchini Ivory Coast, Tisa kati yao wanatoka ligi za Nje ya Afrika na mmoja anacheza ligi ya Afrika Mabululu kutoka Al Ittihad ya Misri

Kwenye mechi 15 za hatua ya Mtoano za AFCON mechi Tano zilienda hatua ya Penati maana ake ni kwamba Washambuliaji walishindwa kumaliza mechi kwenye dakika 90 .

Hii inakupa taswira kuwa Afrika tuna changamoto kwenye eneo la ushambuliaji

Al Ahly wamesajili mshambuliaji raia wa Ufaransa aliyekua anacheza timu kubwa Ujerumani Antony Modeste Lakini nae ameshindwa kuonesha makali yake

Kocha wa zamani wa Al Ahly Mokthar Mokhtar amesema mchezaji huyo sio Level za Al Ahly

Hoja yangu ni kwamba hii ndo nafasi ngumu zaidi kumpata mchezaji Afrika

Sisemi kwamba hakuna Washambuliaji wazuri lakini ni wachache kulingana na mahitaji yaliyopo

Dirisha dogo la usajili tumesajili Washambuliaji wawili Freddy Michael na Pa Omar Jobe

Freddy mpaka sasa amefunga goli 1 na Asist 1 kwenye mechi 6 alizocheza

Jobe amefunga goli 2 kwenye mechi 6.

Mjadala ni je ni Washambuliaji hao ni wazuri au tumepigwa.

Kwa asili ya eneo wanalocheza huwezi kupata majibu ndani ya muda mfupi kama huo

Niwaombe wana Simba wenzangu tuwe wavumilivu, Tuwape muda Washambuliaji wetu ili kuwapunguzia presha.

Sio rahisi kama tunavyodhani kuwa tunaweza kupata mshambuliaji bora na tishio na akaonesha makali yake ndani ya muda mfupi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live