Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahmed Ally awataja walioiharibia hesabu Simba

Ahmed Ally Awatetea Mastraika Simba .jpeg Ahmed Ally.

Wed, 29 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amebainisha maeneo ambayo timu yao ilikosea na kusababisha kushindwa kufanya vizuri kwenye michuano walioshiriki msimu huu ikiwemo Ligi Kuu ya NBC, Kombe la Shirikisho la CRDB na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ahmed amesema hayo jana baada ya Ligi Kuu kutamatika huku Simba wakimaliza nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo ambapo wameangukia kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika ambayo watashiriki msimu ujao jambo ambalo amesema hayakuwa malengo yao kabisa.

“Tunamshukuru Mungu Ligi imemalizika salama japo haijamalizika kwa namna ya kumpendezesha Mwanasimba yeyote lakini hatuna budi kukubali kwa sababu ikishatokea imetokea, maji yakimwagika hayazoleki, hili ni gumu sana na linaumiza.

“Zaidi ya miaka 7 Simba haijashika nafasi ya tatu. Baada ya kukosa Ubingwa tukasema tupambanie nafasi ya pili ili twende Ligi ya Mabingwa, mechi tulizopata sare ndizo zimetuharibia hesabu.

“Mpaka Simba imefika hapa msimu huu ni makosa yetu sisi wenyewe, katika mechi ambazo zilikuwa zinakwenda kuamua jambo flani sisi ndiyo tulizipoteza. Msimu huu umekuwa mgumu sana kwetu. Nafasi ya kwenda kushiriki kombe la Shirikisho haikuwa malengo yetu, malengo yalikuwa Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini tunamshukuru Mungu.

“Yapo maeneo mengi ambayo Simba tunapaswa kwenda kuboresha ili msimu ujao tuwe bora zaidi. Tunawashukuru mashabiki wetu wamekuwa nasi tangu mwanzo wa msimu mpaka leo, wapo ambao hawajakosa mechi hata moja, wametimiza majuku yao kwa asilimia 100 lakini upande mwingine ndio kumekuwa na changamototo.

“Tunakwenda kuangalia wapi tumekosa, msimu huu haukuwa mzuri kila maeneo katika mashindano yote, hivyo lazima tufanye tathmini ya kina kujua tulipokosea ili tuboreshe kuekelea msimu ujao," amesema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live